Jumanne 20 Oktoba 2026 - 07:00
Ni Muhimu Kuhifadhi Vazi la Uwanafunzi Katika Kutafuta Riziki

Hawza/ Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza nchini Iran, amesisitiza umuhimu wa kutatua changamoto za maisha zinazowakabili wanafunzi wa Hawza, akieleza kwamba ni muhimu kuhifadhi, mtindo wa maisha unaolingana na hadhi na maadili ya mwanafunzi wa Hawza wakati wa kuchagua kazi kwa ajili ya kujikimu kimaisha.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kikao maalumu cha Kamati ya Fedha na Uchumi ya Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi na Wanazuoni wa Hawza ya Qum kilifanyika kwa kumshirikisha Ayatullah Araki, ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza nchini Iran, katika kikao hicho washiriki walijadiliana kuhusu hali ya maisha ya wanafunzi wa Hawza na njia za kuboresha hali yao ya kiuchumi pamoja na ile ya familia zao.

Ayatullah Araki, akizungumzia umuhimu wa kuhifadhi hadhi ya wanafunzi wa Hawza, alisisitiza kwamba ni muhimu kuzingatia vazi la uanafunzi wakati wa kuchagua kazi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya maisha. Aidha, alieleza kuwa ni muhimu kuanzisha kamati maalumu itakayoshughulikia uhifadhi wa jambo hili muhimu.

Akisisitiza ulazima wa kuzingatia hali ya maisha na ustawi wa familia za wanafunzi wa Hawza, alisema: “Kuna baadhi ya hatua zinazoweza kutekelezwa kwa lengo la kusaidia kukidhi mahitaji ya maisha ya familia za wanafunzi wa Hawza, na inawezekana kutumia uwezo na fursa zilizopo ndani ya familia zao. Miradi hii, pamoja na kuchangia katika kukidhi sehemu ya mahitaji yao ya kimaisha, itasaidia pia kuondoa changamoto zinazowakabili wanafunzi wa Hawza.”

Mwanzoni mwa kikao hicho, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Barqai, Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi na Wanazuoni wa Hawza ya Qum, aliwasilisha ripoti kuhusu miradi na mipango inayoshughulikiwa na kamati hiyo. Baadaye, wajumbe wa kamati walitoa maoni na mapendekezo yao kuhusu masuala yaliyojadiliwa.

Mwisho wa kikao, ilikubaliwa kwamba kamati hiyo itaandaa mipango ya utekelezaji kwa kuzingatia mapendekezo na maelekezo yaliyotolewa katika kikao hicho.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha